
Baada ya taarifa ya Habari ITV utaona
kuna Kibonzo ambacho huandaliwa na mchoraji Nathan Mpangala, huenda
wengi hatufahamu kuhusu yeye.
Kapata nafasi kuonekana kwenye show ya
Mkasi March 02, ameanza kuzungumzia safari yake ilikoanzia mpaka kuingia
kwenye uchoraji wa katuni; “Baada ya
kumaliza masomo ya Sekondari nikaenda kusoma fine arts.. Baada ya
kumaliza nikajikuta niko tu sielewi nakwenda wapi. Nikajikuta nimeanza
tu kuchora katuni, nakumbuka mchoro wangu wa kwanza ilikuwa kwenye
gazeti la Uhuru.. ilikuwa ni hadithi a michoro, ile michoro imeanza
kutoka mimi sina habari“

Nathan Mpangala
Mother
alivorudi nyumbani akaniambia mwanangu nimeambiwa ofisini kwamba jina
lako limeonekana kwenye gazeti la Uhuru, nilikuwa kama nimezaliwa upya.
Baadaye tukawa na Gazeti la Sanifu ikawa kama kijiji cha wachoraji..
wachoraji tukawa tunakutana wengi tunashare..”

Tofauti ya katuni kwenye gazeti na katuni za kwenye TV; “Tofauti
ya kuchora katuni kwenye gazeti kila siku na kuchora kwenye TV, kwenye
gazeti naweza kuchora mchoro ambao ni fumbo sana lakini kwenye TV
itabidi nichore message ambayo iko clear kwa sababu kuna sekunde kama 35
hivi.. kama nitakuwa nabanabana kama mafumbo tofauti na gazeti mtu
asipoelewa sasa hivi atafika nyumbani atacheki kidogo..”
Ni kitu gani kigumu kwenye kazi yake?; “Katika
vitu vinanipa shida bora unakuja na idea halafu mhariri anakwambia hebu
tafuta nyingine.. Kuliko ile unafika asubuhi ‘Nathan hebu mchore
fulani’, kuchora ni maoni binafsi..”
Sifa za mchora katuni; “Hizi katuni za maoni msingi mkubwa lazima uwe unafuatilia masuala ya kila siku..”
Hapa ametaja baadhi ya watu ambao ni rahisi kuchoreka; “Kama
mtu anakuwa na features ambazo zinaonekana kirahisi ni rahisi
kuchoreka, kwa mfano mwalimu Nyerere.. Mizengo Pinda.. Benjamin Mkapa..”
Kazi ya uchoraji na mazingira ya Uchaguzi mkuu 2015; “Kama
wamiliki wa vyombo vya habari wataamua kutoka kwenye misingi na
taratibu za undeshaji wa vyombo vya habari automatically wanakuja
kuwaathiri wachoraji, maripota. Ilishasemwa kama wewe unamiliki vyombo
vya habari ujiweke pembeni halafu utengeneze Management ikuendeshee
biashara…”

Jinsi alivyoingia ITV kuchora vibonzo vya taarifa ya Habari; “Nilikuwa na wazo hilo.. nilikuwa kwenye mkutano Arusha nikapata simu kutoka kwa Mkurugenzi wa ITV na Radio One,
akasema ukirudi njoo tuonane.. Nilivofika tu nikatia timu. Akasema
nenda kafikirie tunachotaka tuwe na katuni ambayo itakuwa inabeba ujumbe
fulani kila siku ndio ilipoanzia kibonzo..”