GWIJI wa muziki wa Rock Uingereza, Sir Elton John juzi alifunga ndoa
na mpenzi wake David Furnish ikiwa ni miaka tisa tangu Desemba 21, 2005
walipoingia katika uhusiano huo wa watu wenye jinsia moja.
Walifunga ndoa mbele ya wanafamilia, marafiki na wageni wachache walioalikwa huko Windsor nchini England.
Waalikwa wengi wao walikuwa watu maarufu wakiwemo: Familia ya David
na Victoria Beckham, David Walliams na mkewe Lara Stone, Liz Hurley na
mwanaye Damian, waliowasili kwa usafiri wa gari katika eneo la sherehe.
Beckham alikuwasili pia na watoto wake Brooklyn, Romeo, Cruz na Harper. Sir Elton ni baba wa ubatizo wa Brooklyn na Romeo.