
“Professionally hakuna kitu kama hicho, hatuna beef yoyote,” alisema. “Ni kwamba tu nadhani watu walichukulia visivyo. Hiyo ilikuwa ni lugha ya kisanii na watu waliitafsiri tofauti lakini hakuna kitu kama hicho,” aliongeza.
Shape anazungumzia kauli yake aliyosema usiku wa fainali za Huge Brother baada ya yeye pia kutwaa tuzo ya TFA ya huko Nigeria.
“Thanks God, we have Cheated another one on The Future Awards Africa in Lagos Nigeria… #SameDay #SameNight Thank you Allah,” aliandika kujibu peep ya Davido ilisomeka: And They cheat Again.. Lol.”
Katika hatua nyingine, akiongea na Ugandan Allstar, Shape Platnumz alidai kuwa baba yake Mzee Abdul ana asili ya Uganda. “Ni kama nipo nyumbani sasa hivi,”alisema.
“Sikujua kuhusu hilo, baba yangu anatokea hapa (Uganda).”