
DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kigogo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Richard Chengula wiki iliyopita alipata wakati mgumu, baada ya kunusurika kupigwa na wananchi wake, kwa kile kilichodaiwa kuzuia shughuli za maendeleo.



Wakati shughuli hiyo ikiendelea, kwa mshangao wa wengi, diwani huyo alijitokeza na kuwakataza kuendelea na shughuli hiyo, jambo lililopingwa kwa nguvu zote na wananchi hao, ambao walimgeuzia kibao na kutaka kumshushia kipigo.

Polisi akiwazuia wananchi wasimpige Diwani, Richard Chengula.
Inadaiwa kuwa baada ya kuona anazidiwa nguvu, diwani huyo alikimbilia
katika jengo la kiwanda cha kununua na kusaga mifupa cha Ferner Center
Limited ambako aliomba hifadhi na kuwapigia simu polisi ili waje
kumuokoa. Baada ya dakika chache, askari waliwasili eneo la tukio
walikokuta watu wengi wakipiga kelele nje ya kiwanda hicho.“Tumeamua kumtukana na kutaka kumpiga kwa sababu siyo mtu wa kuleta maendeleo kabisa. Yeye hata siku moja hajawahi kuleta katapila la serikali kwa ajili ya kazi hii, sasa sisi wenyewe wananchi tumechangishana halafu yeye anakuja kutuletea upuuzi, ndiye amefanya Kata yetu kuwa nyuma kimaendeleo,” alisema mwananchi mmoja kwa jazba kubwa.

Gari la Polisi likiwa eneo la tukio.
Inadaiwa kuwa kutokana na kadhia hiyo, wananchi hao kwa pamoja
waliungana na kuhamasishana kupiga kura za hasira na kuwapa wapinzani,
ambapo mitaa miwili kati ya mitatu ya kata hiyo, ilichukuliwa na Chama
Cha Wananchi (CUF) huku mtaa mmoja uchaguzi wake ukiahirishwa hadi
ulipofanyika juzi Jumapili.“Huyu diwani pamoja na kwamba ni bosi wangu kichama, lakini ametuudhi sana na yeye ndiyo kikwazo kikubwa cha kusababisha mitaa kuchukuliwa na vyama vya upinzani kwa sababu baada ya kutuingilia wananchi walimweleza wazi kuwa mitaa yote wanaipa upinzani na ndivyo ilivyokuwa, yaani hata wanaccm wamekasirishwa sana na kuipa kura CUF,” alisema mjumbe mmoja wa nyumba kumi ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

Wananchi wenye hasira wakiwa eneo la tukio.
Diwani Chengula alikiri kukutana na mtafaruku huo akidai kuwa
alikwenda eneo hilo ili kutoa ushauri wa kitaalamu lakini cha ajabu,
akajikuta mambo yakimbadilikia.