Stori: Imelda Mtema
STAA wa
filamu Bongo, Wastara Juma, ametamka hadharani kuwa hana uhusiano wa
kimapenzi na msanii yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Wastara alisema
kuna maneno mengi yanasemwa kuwa ana uhusiano na mtu ndani ya kundi
hilo kitu ambacho si sahihi, atamuanika mrithi wa marehemu Sajuki siku
si nyingi.
“Unajua muda utafika tu lakini kwa hivi sasa sina bwana wala sihitaji
mtu yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie na mtu ambaye ataishi na mimi
muda ukifika nitawatambulisha na kila mmoja atamjua na siyo mtu
kunitabiria au kubuni nitamuweka wazi muda si mrefu,” alisema Wastara.