
Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke
wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita
inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi
duniani.
Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko
darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei
anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya
wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.Prissilla alijiunga na shule hii ya 'Leaders Vision Preparatory School' miaka mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika umri wake.
Sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.
Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende shuleni.