Na Gladness Mallya/Amani
MSANII wa filamu Bongo, William Mtitu ameelezea jinsi alivyoteseka usiku kucha kisha kukimbizwa hospitali na kulazwa kwa saa kadhaa baada ya kuzidiwa.
Msanii wa filamu Bongo, William Mtitu akiwa hoi hospitali.
Akizungumza na Amani, Mtitu alisema kuwa hali hiyo ilitokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria usiku wa kuamkia Jumanne ndipo alipelekwa katika hospitali moja iliyopo maeneo ya Magomeni Kagera, Dar alikolazwa.
“Yaani hali yangu ilikuwa mbaya, usiku sikulala kabisa nimejua kweli malaria ni hatari lakini kwa sasa naendelea vizuri baada ya kuwekewa dripu, namshukuru Mungu,” alisema Mtitu.Msanii huyo aliongeza kuwa, anaamini hali yake ilikuwa mbaya kwa kuwa ni nadra sana kusumbuliwa na malaria.
NGANA NASI KATIKA FACEBOOKTWITTER , INSTAGRAM YOUTUBE

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget