Imelda Mtema/mchanganyiko
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Cyrill Kamikaze ‘Cyrill’ na Mbongo Muvi Sabrina Omary ‘Sabby’ hivi karibuni walinaswa katika ufukwe wa Hoteli ya Golden Tulip, Masaki jijini Dar wakiwa kimahaba na hivyo kuzidisha tetesi kuwa wanatoka kimapenzi.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Cyrill Kamikaze ‘Cyrill’ na Mbongo Muvi Sabrina Omary ‘Sabby’ wakipozi kimahaba.
Chanzo chetu makini kilisema wawili hao walionekana hotelini hapo wakiwa eneo la kuogelea na walipomaliza walihamia katika viti ambako sasa walikumbatiana kimahaba kana kwamba hakuna mtu anayewaona.
Kwa nyakati tofauti walipoulizwa kuhusu tetesi za kuwa wapenzi na ushahidi wa picha, kila mmoja alikana, wakidai zitakuwa ni picha za kutengenezwa kwa sababu mchezo huo umekuwa maarufu siku hizi huku Sabby akisisitiza kuwa angefika ofisini ili kujiridhisha na picha hizo ndipo aweze kuzungumza, kitu ambacho hakukifanya.
Hamida Hassan/mchanganyiko
UKARIBU wa mastaa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba maarufu kama Dude na msanii mwenzake Ester Kiama unaonyesha kama kuna kitu kati yao baada ya kuonekana kuwa karibu kwa muda mwingi kiasi kinachotia shaka!
Staa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba maarufu kama Dude.
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimesema mara kwa mara wanaonekana kuwa karibu kila wanapokwenda na kuonyesha dalili zote za kimahaba, lakini wenyewe wanadai ni washkaji walio kazini.
Gazeti hili lilibahatika kuwafuma wakiwa pamoja na walipoulizwa juu ya tuhuma za kujihusisha kimapenzi, kila mmoja alimtupia msalaba wa kujibu mwenzake.  “Mh, jibu wewe, mimi najua Dude ni kaka yangu na ni mfanyakazi mwenzangu”, alisema Ester.
KWAKO mtaalamu wa Hip Hop uliyeibeba Ilala nzima begani, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, mambo vipi mzazi mwenyewe? Uko poa? Mishe zinasemaje?
Ukitaka kujua hali yangu, mimi niko poa na ninaendelea na majukumu yangu ya kujenga taifa kama kawaida na barua hii ni sehemu ya majukumu yangu ya kazi hivyo lazima nikuandikie tu, sina jinsi.
Dhumuni la barua hii kwanza kabisa ni kutaka kukukumbusha kidogo umuhimu wako katika jamii. Sitaki kuamini kwamba hujui umuhimu wako lakini kukumbushana ni muhimu, binadamu tumeumbwa kusahau.
Chid wewe ni mwakilishi mzuri sana wa Muziki wa Hip Hop. Tangu kipindi kile ulichosumbua na wimbo wako wa Dar es Salam Stand Up na nyingine kibao.Ulikuwa hukosei, ulikuwa unaachia jiwe baada ya jiwe na kila mtu alikuwa anakubali uwezo wako.
Kudhihirisha wewe ni mkali, nakumbuka ulikuwa ni lulu katika suala zima la kolabo. Wasanii walikuwa wakipanga msururu kukusaka, waliamini ukiingiza sauti yako katika nyimbo zao basi nazo zitakuwa tamu kama mcharo.
Hilo halikuwa na kificho, ulifanya kolabo nyingi sana. Nyimbo kama Neila ya Tunda Man, Hao na nyingine kibao zilinoga sana pale ulipoingiza sauti yako yenye mamlaka ambayo ulijua kuipangilia na kuendana na biti, wewe ni mkali aisee!
Pamoja na uzuri huo, juzikati hapa liliingia suala la wewe kunaswa na madawa ya kulevya. Binafsi sikushtuka sababu dalili za wewe kutumia nilishaziona kabla.Niliona dalili kutokana na matendo yako, yalikuwa hayafanani na uwezo wako mkubwa wa kutunga mashairi yenye uzito. Matukio kama yale ya kumdunda msanii mwenzako, Rehema Chalamila ‘Ray C’, nilijua kabisa si wewe.
Lilipokuja kutokea lile la kukamatwa na madawa pale Air Port, nilisikitika sana kama shabiki wako. Suala la wewe kuanza kuingizwa kwenye mikono ya sheria ni kuzidi kudidimiza kipaji chako na muziki wako kwa jumla.
Nilifuatilia kwa makini kesi yako hadi pale ulipotakiwa kulipa faini nikasema ni jambo la heri lakini unapaswa sasa kubadilika kweli na kutokubali kurudi nyuma. Uliwahi kukiri kuwa unatumia madawa, ukaahidi kuacha lakini ukarudia.
Nikushauri, mimi pamoja na mashabiki wengi Bongo na nje tunakupenda na tunahitaji kuendelea kusikia ‘madini’ yako.Ngoma yako ya Kimbiza ambayo haina muda mrefu sana tangu uiachie inatosha kuonesha kwamba uwezo unao, tupe raha kama ile ambayo ulikuwa unatupa.
Achana kabisa na madawa ya kulevya, sitegemei kukuona tena unakamatwa au unahusishwa katika suala hilo kwa namna yoyote.Ni matumaini yangu utabadilika kweli, kwa leo ni hayo, kila la kheri!
Shani Ramadhani/Mchanganyiko
MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki na filamu nchini, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, ameendeleza tabia yake ya kumpa vipigo vya mara kwa mara mpenzi wake, Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambaye pia ni msanii.
Mwanadada anayefanya vizuri katika muziki na filamu nchini, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Habari kutoka vyanzo vya kuaminika vinasema Shilole alimdunda kwa mara nyingine Nuh wiki iliyopita, baada ya kutokea kutoelewana baina yao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
“Ninampenda sana mume wangu na ninamheshimu, hili suala linapozungumzwa au kuulizwa linaniumiza sana, haya ni mambo ya muda mrefu na yameshamalizika,” alisema msanii huyo nyota wa kibao cha Malele.
Kwa upande wake Nuh alipotafutwa, simu yake haikupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu jambo hilo pia hakujibu.Hii siyo mara ya kwanza kwa wapenzi hao kukwaruzana, kwani imeshawahi kutokea siku za nyuma hadi kufikia wakati wakatengana.
Musa Mateja/Risasi Mchanganyiko
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuwepo madai ya kudaiwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 800 na serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
ILIKUWAJE?
Mwishoni mwa wiki iliyopita, barua inayodaiwa kuandikwa na mamlaka hiyo halali ya serikali, ilisambazwa mitandaoni, ikielezwa kuwa ilikuwa imetumwa kwa meneja wa msanii huyo ambaye kwa sasa ndiye yupo juu, ikimtaka kupeleka nakala za mikataba yote ya muziki aliyoingia kwa ajili ya kufanya shoo, kuanzia mwaka 2010 hadi sasa.
GUMZO MITANDAONI
Baada ya kuwekwa kwa barua hiyo mitandaoni, watu mbalimbali walitoa maoni yao walionyesha hisia tofauti, baadhi wakipinga kwa madai kuwa wanamuonea huku wengine wakisema siyo Diamond tu, bali wasanii wote wanastahili kulipa kodi kutokana na mapato wanayopata kupitia kazi zao.
KODI ZIPOJE KIBONGOBONGO?
Mtaalam mmoja wa mambo ya kodi aliyezungumza na Risasi Mchanganyiko, alisema kwa mujibu wa taratibu zao, msanii huyo anastahili kulipa kodi kiasi cha asilimia kumi ya fedha anazopata katika kila mkataba anaoingia.
“Kuna walipa kodi wengine kama wafanyabiashara, hawa wanalipa kile ambacho kitaalamu kinajulikana kama Capital Gain, yaani kulipa kadiri unavyopata. Mtu anakwenda TRA mwenyewe na kueleza mapato yake na mamlaka itampangia kiasi cha kulipa. Ila watu kama wasanii na wengine wanaolipwa, wanatakiwa kutoa asilimia kumi ya malipo,” alisema mtaalam huyo aliyekataa kutajwa jina gazetini.
DIAMOND ANADAIWA SH. NGAPI?
Kama suala hilo litafanyika kwa mujibu wa mtaalam huyo, Diamond ambaye malipo yake kwa shoo moja yanatajwa kuwa ni shilingi milioni 20 kwa sasa, atatakiwa kulipa kiasi kinachozidi milioni 800 kutokana na hesabu zilizofanywa na watu wanaofuatilia muziki wake.
“Jamaa anafanya wastani wa shoo kama tatu kwa mwezi hapa nyumbani (Tanzania) na tatu zingine nje. Zile za nje analipwa siyo chini ya dola 25,000 kwa shoo moja. Nadhani unajua kwa sasa huyu dogo ndiye anakimbiza sana katika soko, yupo juu na kila promota anahitaji huduma yake,” alisema mdau huyo wa Bongo Fleva.
MCHANGANUO ULIVYO
Kama hesabu za mdau huyo zitakuwa sawa, inamaanisha kuwa Diamond anaingiza wastani wa shilingi milioni sitini kwa mwezi hapa nyumbani, na milioni 127  kwa mikataba ya nje ya nchi (Dola moja ya Marekani ni sawa na shilingi 1700), ikimaanisha kuwa kwa mwezi mmoja, kijana huyo aliyekulia Tandale, anaingiza kiasi cha shilingi milioni 187.5.
JUMLA  YA MAPATO MIAKA MINNE
Kwa mahesabu hayo, Diamond Platnumz anaingiza wastani wa shilingi bilioni 2.2 kwa mwaka, fedha ambayo ukijumlisha kwa miaka minne, ameweka kibindoni shilingi za kitanzania bilioni 8.8, ambazo asilimia kumi yake ni shilingi milioni 880, ambazo ndizo zinazotakiwa kulipwa.
MENEJA AFUNGUKA
Mmoja wa mameneja wa Diamond, Babu Tale alipotafutwa na gazeti hili na kuulizwa kama ni kweli alipewa barua au kujua kuwa barua hiyo ipo, alikataa kulizungumzia suala hilo, akisema siyo jambo la kulielezea kwenye vyombo vya habari.“Hata mimi nimeiona hiyo barua (anautaja mtandao wa kijamii maarufu sana nchini), sina cha kuelezea kwenye media,” alisema meneja huyo huku akikataa katakata kusema kama ameipata au la.
DIAMOND MWENYEWE SASA
Baadaye Risasi Mchanganyiko liliwasiliana moja kwa moja na Diamond mwenyewe, ambaye alikuwa nchini Nigeria, alikoenda kwa ajili ya shoo iliyoandaliwa na Africa Magic Viewers Choice Awards jijini Lagos, alishtuka sana na kuomba asizungumzie suala hilo.“Daah! Milioni 800? Anyway naomba nisizungumzie suala hilo kwa sasa.”
TRA WAIKANA BARUA
Gazeti hili lilipomtafuta ofisa wa TRA, ambaye jina lake limeandikwa katika barua hiyo, aitwaye Tillya V.M. T, alikanusha kuandika barua hiyo na kusema ni mambo ya kugushi yanayofanywa mitandaoni.
“Hakuna kitu kama hicho, its something created,” alisema bosi huyo akimaanisha kuwa jambo hilo ni la kutengenezwa.
NYOTA YA WEMA YAHUSISHWA
Wakati hayo yakijiri, baadhi ya wadau wamesema suala hilo linahusishwa na mojawapo ya kauli iliyowahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu kuwa mwanaume yeyote anayekuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi, nyota yake hung’aa, lakini anapoachana naye, hufifia.
WENGINE WAMHUSISHA ZARI
Aidha, wadau wengine walisema ishu hiyo huenda imeibuka kama mkosi uliochangiwa na kujiingiza katika mapenzi na mwanadada raia wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye mashabiki wanadai ni mtu mwenye mikosi, kwani Diamond ni mwanaume wake wa nne  watoto wote ni ni wa Ivan.
103
Add caption
Niliwahi kuuliza kwa watu wa nguvu shilingi milioni 75 wakipata watatumia kwenye nini?, majibu ya wengi yalikua ni kujenga nyumba na kununua gari huku wengine wakisema watawekeza kwenye biashara.
Sasa basi, pamoja na hiyo milioni 75 kuonekana inaweza kufikiriwa kufanya mambo hayo makubwa ya kimaisha… imefahamika kiwango hicho cha pesa kinaweza kuishia kwenye kununua TV moja tu hii mpya ya Samsung ya inch 85 na usirudishiwe chenchi.
millardayo.com ilipotembelea duka lao Mlimani City, imeambiwa TV hii ina vitu vingi vya kipekee ikiwemo kutumia ishara ya mkono, sauti, na sura kufanya setting mbalimbali ikiwemo kupunguza sauti badala ya kutumia remote.
104
Smart contents mfano Instagram, twitter, facebook na apps nyingine mbalimbali ambapo unaweza kutumia Internet kuwasiliana kwenye mitandao mbalimbali kama vile skype ambapo mnaweza kuonana zaidi ya watu watatu kwa wakati mmoja.
Ina music system yenye mziki mzito hapohapo hivyo ukiwa nayo huna haja ya kununua home theatre, pia faster speed squad core processor.
Digital tuner unaweza kupata local free channels zaidi ya 40 bila decorder na ukitaka channel za kulipia utatumia smart card ambayo unaiweka kwenye smart card slot nyuma ya TV yako.
Vilevile ukiwa na samsung smart phone unaweza kuiunganisha na TV ukaplay videos, music video games kutoka kwenye simu yako.
1. Bishop T. D Jakes
 
Bishop Jakes lives in a $1,700,000 mansion, he has been called America’s best preacher and has been featured on the cover of TIME magazine. He is a writer, preacher and movie producer. Thomas Dexter “T. D.” Jakes, Sr. is the bishop/chief pastor of The Potter’s House, a non-denominational American mega church, with 30,000 members, located in Dallas, Texas. T.D Jakes wears custom made suits and sports a diamond ring the size of a coin. This man of God has been endowed with a $150 million net worth.
2. Bishop David Oyedepo
 
Bishop David Oyedepo is a Nigerian Preacher, Christian Author, Founder and Presiding Bishop of Winners Chapel known as Living Faith Church World Wide. Has been hailed as the wealthiest preacher in Nigeria with a total net worth of $150 million and properties like 4 private jets and homes in the United States and England. After the foundation of the Living Faith Outreach Ministry in 1981, it has evolved to be one of the largest congregations in Africa and has a flourishing mission in Nairobi.
3. E A Adeboye
 
This messenger of God was listed in an African magazine, NEWSWEEK, as the most powerful man in Africa and one of the top 50 global power elites in 2008/2009, among others such as President Barack Obama and Nicolas Sarkozy. Pastor Adeboye heads the Redeemed Christian Church of God (RCCG), something he has done for the last 28years.Amongst his possessions are private jets.
4. Benny Hinn
 
Israeli televangelist,Toufik Benedictus “Benny” Hinn has an estimated net worth of $42 million. He is best known for his regular “Miracle Crusades” – revival meeting/faith healing summits that are usually held in large stadiums in major cities, which are later broadcast worldwide on his television program, “This Is Your Day”. Hinn was born on December 3, 1952
5. Chris Oyakhilome
This is the man behind Believers’ Loveworld Ministries, a.k.a Christ Embassy.His church has an estimated net worth of $30 million – $50 million last year, the charismatic preacher was at the center of a $35 million money laundering case in which he was accused of siphoning funds from his church to foreign banks.
6. Creflo Dollar
 
American Bible teacher, pastor, and the founder of World Changers Church International, Creflo Dollar, has an estimated net worth of $27 million. As his name suggests, this preacher’s “manna” comes in form of the green buck.
7. Kenneth Copeland
 
He runs Kenneth Copeland Ministries, was one of several televangelists whose finances were investigated from 2007 to 2011 by Republican Sen. Charles Grassley of Iowa.
According to an article by the Associated Press that ran in 2008, “His ministry’s 1,500-acre campus, behind an iron gate a half-hour drive from Fort Worth includes a church, a private airstrip, a hangar for the ministry’s $17.5 million jet and other aircraft, and a $6 million church owned lakefront mansion.
The article later added that while Copeland has not released up-to-date salary statements, “the church disclosed in a property-tax exemption application that his wages were $364,577 in 1995; Copeland’s wife, Gloria, earned $292,593. It’s not clear whether those figures include other earnings, such as special offerings for guest preaching or book royalties.”
8. Billy Graham
 
American evangelical Christian evangelist, William Franklin “Billy” Graham, Jr., has a net worth of $25 million. The Southern Baptist evangelist rose to celebrity status as his sermons started getting broadcast on radio and television. Graham was born on a dairy farm near Charlotte, North Carolina in 1918, he has conducted many evangelistic crusades since 1948 . He is now a world renowned televangelist raking in millions of dollars.
9. Matthew Ashimolowo
 
Ashimolowo, the owner of Kingsway International Christian Centre (KICC) gets an annual income of $200,000. Having his humble beginnings as a priest in Foursquare Gospel Church, a Nigerian church that sent Ashimolowo to open a satellite branch in London. Pastor Matthew had other ideas and decided to set up his own church instead. Today, his Kingsway International Christian Center is reportedly the largest Pentecostal church in the whole of the United Kingdom
10. Temitope Joshua
 
Synagogue Church Of All Nations (SCOAN) has an estimated net worth: $10 million – $15 million Nigeria’s most controversial clergyman is also one of its richest and most philanthropic. T.B Joshua heads the Synagogue Church of all Nations (SCOAN), a congregation he founded in 1987, which accommodates over 15,000 worshippers on Sundays.
Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe leo.
Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo.
Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari.
Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,  Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama  kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo  kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani
“Hivyo,  kwa mujibu wa sheria za chama, Zitto alikiuka sheria  anapaswa kuvuliwa uanachama wake,” alisema Lissu.
Lissu aliongeza kuwa hata kama Zitto angeweza kwenda kushitaki lazima angeanzia katika mahakama ndogo za wilaya yaani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi au Masijala ya Mahakama ya Wilaya  tofauti na alivyopeleka kesi hiyo moja kwa moja Mahakama Kuu.
Mahakama hiyo pia imemtaka mbunge huyo wa zamani kukilipa chama hicho gharama zote za kesi hiyo kama ilivyoelekezwa na mahakama, na kwa mujibu wa Lissu,  Chadema kitakaa na kutathmini gharama husika.
Kuhusu utambulisho wa Zitto bungeni, Lissu alisema  kwa mujibu wa kanuni za chama chake, katibu wa chama chake anatakiwa kumwandikia barua Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kumjulisha  Zitto tena si mwanachama wao na taratibu zingine zitafuatia.
Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, akiwa na mume wake, Emmanuel Mbasha.
KESI ya kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa siri.
Kesi hiyo ilianza kuunguruma kwenye ofisi ya hakimu (Chamber), mishale ya saa 5 hadi saa 8 mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama wa Wilaya ya Ilala, Flora Mjaya ambapo shahidi namba tatu, Flora aliitwa kutoa ushahidi wake. Kesi hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga na imeahirishwa hadi Aprili 16, mwaka huu.
Siku hiyo, shahidi namba nne ambaye ni daktari anatarajiwa kutoa ushahidi wake na mshitakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana. Mbasha anashtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji, la kwanza anadaiwa kulifanya Mei 23, mwaka jana, eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na Mei 25, mwaka jana akidaiwa kutenda kosa hilo kwa binti huyo kwa mara nyingine eneo hilohilo.
Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
KWELI ni maajabu! Yule mgonjwa ambaye mpaka sasa, madaktari hawataki kumtaja jina, aliyelazwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Dar baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa rundo la vyuma tumboni, maajabu saba yameibuka, Uwazi  linakupa zaidi.
Tukio hilo la kihistoria lilitokea wiki iliyopita  ambapo mgonjwa huyo alifikishwa Muhimbili akitokea Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha, Pwani.
Mgonjwa ambaye mpaka sasa, madaktari hawataki kumtaja jina, aliyelazwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Dar baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa rundo la vyuma tumboni.
Kwa mujibu wa ndugu mmoja ambaye hakupenda jina lake lichapwe gazetini, vyuma mbalimbali vilivyotolewa tumboni kwa mgonjwa huyo vinaunga moja kwa moja na mambo ya ushirikina.

AJABU NAMBA MOJA
Ndugu huyo alisema kuwa, mgonjwa wake alikuwa akienda chooni bila shida ambapo baada ya kutolewa vitu hivyo, wengi  walitarajia alikuwa hapati choo jambo ambalo si la kweli.
Rundo la vyuma vilivyotolewa tumboni madaktari.
AJABU NAMBA MBILI
“Kuna sauti ya mwanamke ilikuwa ikimwita mara kwa mara bila kujulikana ni nani wala kuonekana. Ndiyo maana tunaamini kuwa, vitu vile kuwa tumboni mwake kulitokana na mambo ya kishirikina,” alisema ndugu huyo.

AJABU NAMBA TATU
Ilielezwa na ndugu huyo kwamba, kabla mgonjwa huyo hajajulikana ana matatizo gani alikuwa akisikia uzito mkubwa ndani ya tumbo hali iliyokuwa ikimfanya ahisi amebeba zigo f’lani.
“Yeye mwenyewe alikuwa akisema ana kitu tumboni, aliamini ana uvimbe mkubwa sana kwani ulikuwa ukitikisika wakati wa kutembea lakini kudhani ni vyuma, wala,” alisema ndugu huyo.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligalesha akiangalia vyuma hivyo.
AJABU NAMBA NNE
Katika hali ya kushangaza, mgonjwa huyo aliweza kula ugali kiasi kikubwa sana licha ya tumboni mwake kuwa na mzigo mkubwa wa vyuma.

AJABU YA TANO
“Kuna mzee mmoja kule Kibaha anakoishi alikuwa akimwambia mara kwa mara kwamba anatakiwa kwenda hospitali kupima afya yake kwani mwonekano wake ulikuwa ukitoa tafsiri kwamba, ndani ya mwili wake si kuzuri lakini alikuwa akipuuzia kwa kuamini hali aliyonayo angepona kawaida tu. Ni ajabu sana, sijui yule mzee alikuwa akimwonaje?” alisema ndugu huyo.

AJABU NAMBA SITA
Ndugu: “Kikubwa ni kwamba, licha ya mzigo wote ule wa vyuma kuwepo tumboni, lakini alikuwa akipata usingizi kama kawaida. Na ilikuwa ili apate usingizi lazima alale chali (kuangalia juu).
“Hapo usingizi ni mpaka asubuhi. Lakini kusema ukweli kwa mzigo ule wa vyuma tumboni bado ni ajabu, ilitakiwa asilale kabisa.”
Akiendelea kufanya uchunguzi wake.
AJABU NAMBA 7
Hili ndilo ajabu kubwa kuliko yote, kwani ndugu huyo alisema mpaka sasa anashindwa kufahamu vyuma vile viliingiaje ndani ya tumbo la mgonjwa huyo kwa vile, vyuma hivyo vingi haviwezi kupita kwenye koo kwenda tumboni.

ALIFIKAJE MUHIMBILI
Ndugu huyo alisema kuwa, mgonjwa wake alikuwa akitumia dawa za asili Kibaha lakini hali ilivyozidi kuwa mbaya, aliamua mwenyewe kwenda Hospitali ya Tumbi na baadaye Muhimbili.
“Alipofika Tumbi madaktari walimshauri aje Muhimbili kwa uchunguzi na kisha matibabu. Baada ya kufika alifanyiwa  uchunguzi wa kina kwa kupigwa X-ray haraka ambapo alibainika ana tatizo  kubwa tumboni na kuwalazimu  kumfanyia upasuaji.

Bado madaktari wa Muhimbili wanashangazwa na wingi wa vyuma walivyovikuta ndani ya tumbo la mgonjwa huyo na jinsi ilivyoingia, kwani ni sayansi nyingine kabisa.

KILICHOKUTWA
Vyuma vilivyokutwa ndani ya tumbo la mgonjwa huyo ni misumari, bisibisi, nondo iliyopinda, plagi ya gari, mkufu na kanda ndefu ya kaseti.
Vyuma vingine ni vipande vya mawe, pini, funguo za vitasa vya milango ya nyumba, kasha ya risasi na kifaa cha kubania wembe kwa vinyozi.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligalesha alisema mgonjwa huyo jina lake  linaendelea kuhifadhiwa na kukiri alifika hapo wiki tatu zilizopita akitokea Tumbi.
“Ndugu waandishi kama mnavyoona, mgonjwa  huyu alikuwa  na taizo  kubwa  si  jambo la kawaida  mwanadamu  kuishi na vyuma tumboni. Upasuaji wake ulichukua saa mbili na nusu,” alisema  msemaji huyo.
Naye mganga wa tiba ya kienyeji, maarufu maeneo ya Kigogo, Dar alipoulizwa na Uwazi ni vipi vyuma vinaweza kuingia kwenye tumbo la binadamu, alisema:
“Kwanza mtu asije akadhani yule mgonjwa alikula vile vyuma. Ule ni utamaduni kafanyiwa. Vyuma vinaingizwa tumboni kwa njia ya kishirikina na kukaa humo kwa muda mrefu.
“Kinachotokea wakati vyuma vikiingia tumboni mtu anaweza kujisikia kuwashwa tumbo na kujikuna kila mara. Mara nyingi mambo hayo hufanywa na mtu ambaye ni mbaya wako, kwa kukuendea kwa waganga au kwa wachawi,” alisema mganga huyo.
Mwandishi Wetu
Haya ni madai mazito! Mama mzaa chema wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu anadaiwa kumzaba vibao askari wa kampuni binafsi.
Mama mzaa chema wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu.
UJIUNGE NA SHUHUDA
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi lilijiri kwenye Bandari ya Dar es Salaam, majira ya mchana Ijumaa iliyopita.Kabla ya kushusha stori kamili, Ijumaa Wikienda lilimhoji shuhuda huyo kama anamjua vizuri mama Wema ambapo alithibitisha kuwa ni yeye huku akisapotiwa na wenzake waliokuwa wakisikika kwenye simu.
KUMBE ALIFUATANA NA WEMA
“Nani asiyemjua mama wa staa mkubwa kama Wema? Tena kafuatana na Wema mwenyewe. Kila mtu hapa anamjua ngoja tujaribu kupata picha zake nzuri,” alisema shuhuda huyo kwa kujiamini.
Shuhuda huyo alidai kwamba chanzo cha yote, mama Wema alidaiwa kutumia mlango usio sahihi na alipofuatwa kuelekezwa ndipo likaibuka timbwili zito.
ALIKUWA ANATOKEA WAPI?
“Kinachoonekana alikuwa ameshuka kwenye boti akitokea Zanzibar kwenye shughuli binafsi. Wakati anatoka kuchukua hamsini zake akiwa na Wema, wakapita mlango ambao siyo sahihi.
“Sasa askari wa kampuni binafsi akawafuata na kuwazuia ili kuwapa maelekezo lakini mama Wema alikasirika, akaanza kumpiga vibao.
“Hapo ndipo lilipoibuka timbwili zito kwani askari naye hakutaka kukubali kirahisi.
“Naye mama Wema kuonesha si mtu wa mchezo aligeuka mbogo na kusababisha watu kushindwa kuamini.
MAMA WEMA KAPITIA JESHINI?
“Yaani swali kubwa kila mtu alikuwa anahoji kama mama Wema amepitia jeshini kwa jinsi alivyoonekana ngangari.“Kiukweli yule mama siyo wa kumchezea anaonekana yupo vizuri kimazoezi.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
WAMALIZANA POLISI
“Baadaye walipelekana kwenye kituo cha polisi cha pale bandarini wakamalizana lakini tayari ishu hiyo ilishageuka gumzo maeneo hayo.“Hatujui walikubaliana nini zaidi ya kuwaona wakitimua zao kwani hawakutaka kukusanya tena watu,” alidai shuhuda wetu huyo.
MAMA WEMA AOMBA APUMZIKE
Baada ya kumwagiwa tukio hilo la moto, gazeti hili lilimtafuta mama Wema ambaye hakukanusha kutokea kwa tukio hilo badala yake aliomba aachwe kwanza apumzike nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar.
“Niache nipumzike kwanza nitakusimulia tukio,” alisema mama Wema.Alipotafutwa kwa mara nyingine hakuwa tayari kutoa ushirikiano hivyo jitihada za kusikia upande wake zinaendelea.
WEMA VIPI?
Kwa upande wake Wema, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa ikielezwa kwamba alikuwa amebanwa na
Gladness Mallya/ijumaawikienda
Inasikitisha sana! Huku akitundikiwa dripu nyumbani kwao, Sinza ya Vatican jijini Dar, daktari ameanika ugonjwa unaomtesa staa wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ kuwa vipimo vinaonesha anashambuliwa na fangasi kichwani (ubongo) na shingoni.
Staa wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
YU HOI TENA
Habari zinaeleza kuwa tatizo hilo limesababisha Banza kuwa hoi kwa mara nyingine akiumwa na kichwa kupita kiasi hivyo kushindwa kufanya lolote.Kufuatia maumivu anayoyapata, Banza amewaomba Watanzani wamuombee kwani anaamini katika maombi yao.
MAOMBI MUHIMU
Akizungumza kwa tabu na Ijumaa Wikienda, Banza ambaye kwa sasa hawezi kunyanyuka kwenye kochi alisema anatamani angepona ili arudi jukwaani hivyo maombi yao ni muhimu kuliko kitu chochote na ni msaada tosha kwake.
“Kikubwa nawaomba Watanzania waniombee kwani hali niliyonayo siyo ya kawaida, nasikia maumivu makali sana ya kichwa na shingo hadi nashindwa kula.“Hata kuongea ndiyo hivi kwa shida na muda mwingi naweka kitambaa cha maji ya baridi kwenye paji la uso ili kupunguza makali ya maumivu,” alisema Banza kwa masikitiko makubwa.
Banza kwa sasa anatibiwa nyumbani kwao baada ya kupata matibabu kwenye Hospitali ya Sinza-Palestina ambapo anaongezewa maji (dripu) na kuendelea kumeza dawa za ugonjwa huo.
DAKTARI ATHIBITISHA
Banza alisema ugonjwa huo amethibitishiwa na daktari wake kwenye hospitali hiyo baada ya kuchukuliwa vipimo.
FANGASI KICHWANI AU KWENYE UBONGO IKOJE?
Kwa mujibu wa mtaalam wa magonjwa ya kichwa, kitaalam ugonjwa huo huitwa Mucormycosis.
Ni ugonjwa ambao katika siku za hivi karibuni umekuwa maarufu huku ukisababisha vifo vya watu wengi. Kitaalam, ugonjwa huu husababishwa na fangasi waitwao Murcorales ambao huingia ndani ya mwili wa binadamu kwa njia ya hewa.
Ukivuta hewa yenye fangasi hao, huingia na kwenda moja kwa moja kwenye mfumo wa damu kisha kuanza kuzunguka ndani ya mwili kufuata damu. Baada ya kukaa kwa wiki kadhaa kwenye mfumo wa damu, huhamia kwenye uti wa mgongo (spinal) ambapo huzaliana kwa wingi na kuanza kusambaa kuelekea kwenye ubongo.
Fangasi hawa wanapofika kwenye ubongo, huushambulia na kusambaa kwa kasi ambapo uwezekano wa mgonjwa kupona huwa mdogo. Kati ya kila watu 100 wenye ugonjwa huo, karibu 30 hupoteza maisha.
DALILI ZA UGONJWA
Dalili za awali za ugonjwa huo ni kuwa na uvimbe mwekundu unaotokea kuzunguka macho ambao huongezeka kadiri fangasi wanavyozidi kushambulia ubongo.
Dalili nyingine ni pamoja na kuumwa kichwa upande mmoja, uso kuuma, homa kali, kupumua kwa shida na kutokwa kamasi za rangi nyeusi.Pia ngozi ya mwili wa mgonjwa huanza kubadilika rangi na kuwa nyekundu. Hali hiyo huendelea hadi ngozi inapobadilika zaidi na kuwa nyeusi.
TIBA
Vipimo vya ugonjwa huo hufanywa kwa mashine ya MRI ambapo mtu akibainika ameambukizwa fangasi hao, hutibiwa kwa upasuaji wa ubongo na kuondoa sehemu zilizoathirika pamoja na kutumia dawa kali za Amphotericin B au Posaconazole, wakati mwingine dawa hizi huchanganywa pamoja.
WATU WALIOPO KWENYE HATARI
Watu wanaoweza kuupata ugonjwa huu kwa urahisi ni wagonjwa wa kisukari, HIV, waliofanyiwa upasuaji wa kupandikiza viungo ndani ya miili yao kama figo au ini, na matumizi ya dawa za ‘corticosteroids’ kwa kipindi kirefu.
Hamida Hassan/ijumaawikienda
Kha! RB namba KTN|RB/11213/2014 –UTAPELI inamsaka msanii wa muziki na sinema za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ tangu mwaka jana, akidaiwa ‘kuchikichia’ nguo za shilingi laki saba, mali ya aliyekuwa Mtangazaji wa EATV,  Nasra Dattani ‘Lady Naa’ ambaye alimkabidhi begi lake la nguo baada ya kumaliza kurekodi filamu iitwayo Catherine.
Msanii wa muziki na sinema za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Lady Naa alisema kuwa alimvumilia Hemed kwa muda mrefu kwani alimpa mzigo huo na kumuomba akaushushe dukani kwa rafiki yake maeneo ya Kinondoni lakini hakufanya hivyo na alipokuwa akimkumbusha alikuwa akimwambia kuwa atampelekea.
“Kila nikikutana naye nilikuwa namuomba anirudishie anasema nifanye lolote na kinachonishangaza amezipeleka wapi maana mle kulikuwa na nguo za kike ambazo nilizitoa Uingereza,” alisema Lady Naa.
Alidai kwamba baada ya kumzungusha kwa muda mrefu ndipo alipoamua kumfungulia kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama, Dar ambapo hadi leo anasakwa. Baada ya habari hizo kulifikia gazeti hili, mwanahabari wetu alimwendea hewani Hemed lakini namba yake haikupatikana hivyo jitihada zinaendelea.
mKAASI I III
Baada ya taarifa ya Habari ITV utaona kuna Kibonzo ambacho huandaliwa na mchoraji Nathan Mpangala, huenda wengi hatufahamu kuhusu yeye.
Kapata nafasi kuonekana kwenye show ya Mkasi March 02, ameanza kuzungumzia safari yake ilikoanzia mpaka kuingia kwenye uchoraji wa katuni; “Baada ya kumaliza masomo ya Sekondari nikaenda kusoma fine arts.. Baada ya kumaliza nikajikuta niko tu sielewi nakwenda wapi. Nikajikuta nimeanza tu kuchora katuni, nakumbuka mchoro wangu wa kwanza ilikuwa kwenye gazeti la Uhuru.. ilikuwa ni hadithi a michoro, ile michoro imeanza kutoka mimi sina habari
mKAASI I IV
Nathan Mpangala
Mother alivorudi nyumbani akaniambia mwanangu nimeambiwa ofisini kwamba jina lako limeonekana kwenye gazeti la Uhuru, nilikuwa kama nimezaliwa upya. Baadaye tukawa na Gazeti la Sanifu ikawa kama kijiji cha wachoraji.. wachoraji tukawa tunakutana wengi tunashare..
mKAASI I
Tofauti ya katuni kwenye gazeti na katuni za kwenye TV; “Tofauti ya kuchora katuni kwenye gazeti kila siku na kuchora kwenye TV, kwenye gazeti naweza kuchora mchoro ambao ni fumbo sana lakini kwenye TV itabidi nichore message ambayo iko clear kwa sababu kuna sekunde kama 35 hivi.. kama nitakuwa nabanabana kama mafumbo tofauti na gazeti mtu asipoelewa sasa hivi atafika nyumbani atacheki kidogo..
Ni kitu gani kigumu kwenye kazi yake?; “Katika vitu vinanipa shida bora unakuja na idea halafu mhariri anakwambia hebu tafuta nyingine.. Kuliko ile unafika asubuhi ‘Nathan hebu mchore fulani’, kuchora ni maoni binafsi..
Sifa za mchora katuni; “Hizi katuni za maoni msingi mkubwa lazima uwe unafuatilia masuala ya kila siku..
Hapa ametaja baadhi ya watu ambao ni rahisi kuchoreka; “Kama mtu anakuwa na features ambazo zinaonekana kirahisi ni rahisi kuchoreka, kwa mfano mwalimu Nyerere.. Mizengo Pinda.. Benjamin Mkapa..
Kazi ya uchoraji na mazingira ya Uchaguzi mkuu 2015; “Kama wamiliki wa vyombo vya habari wataamua kutoka kwenye misingi na taratibu za undeshaji wa vyombo vya habari automatically wanakuja kuwaathiri wachoraji, maripota. Ilishasemwa kama wewe unamiliki vyombo vya habari ujiweke pembeni halafu utengeneze Management ikuendeshee biashara…
mKAASI I II
Jinsi alivyoingia ITV kuchora vibonzo vya taarifa ya Habari; “Nilikuwa na wazo hilo.. nilikuwa kwenye mkutano Arusha nikapata simu kutoka kwa Mkurugenzi wa ITV na Radio One, akasema ukirudi njoo tuonane.. Nilivofika tu nikatia timu. Akasema nenda kafikirie tunachotaka tuwe na katuni ambayo itakuwa inabeba ujumbe fulani kila siku ndio ilipoanzia kibonzo..
capt KombaKifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kapteni John Komba ambaye amefariki dunia akiwa hospital ya TMJ February 28 kilitanguliwa na kitu ambacho kinadhaniwa kama kilikua ni ishara ya siku yake ya mwisho.
Claudia John Komba ambaye ni mtoto wa 9 kati ya watoto 11 wa marehemu John Komba ameongea na millardayo.com na kuelezea baadhi ya vitu ambavyo kwao imekua kama kauli ya mwisho kutoka kwa Baba yao ambayo aliitoa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.
Claudia amesema >>>‘Taarifa ilinifikia mida ya saa 9 akasema anajisikia vibaya ambapo wakati yupo njiani akawa anaweweseka sana, tulipofika TMJ hospital walipofanya vipimo walisema ameshafariki’
millardayo.com Kabla ya hapo kulikua na ripoti ya mzee kuugua?
Claudia John Komba: ‘Zilikuwepo baba alikua amekaa ilikua mida ya asubuhi akawa analalamika anajisikia vibaya tukampeleka hospitali, tukagundua sukari imepanda sana na presha imepanda sana, akatolewa akawa anaendelea vizuri’
‘Juzi tarehe 26 february ilikua siku yangu ya kuzaliwa, akaita watoto wote akasema nataka kufanya birthday sababu birthday nyingi huwa zinanipita nakua nipo nje, akatukusanya watoto wote, aliongea maneno ya mwisho akatusihi watoto tupendane tusiweke  matabaka kwamba huyu mdogo huyu mkubwa alisema yeye hana mkataba na Mungu’.

R.I.P Captain John Komba

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget