Shani Ramadhani/Mchanganyiko
MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki na filamu nchini, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, ameendeleza tabia yake ya kumpa vipigo vya mara kwa mara mpenzi wake, Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambaye pia ni msanii.
Mwanadada anayefanya vizuri katika muziki na filamu nchini, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Habari kutoka vyanzo vya kuaminika vinasema Shilole alimdunda kwa mara nyingine Nuh wiki iliyopita, baada ya kutokea kutoelewana baina yao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
“Ninampenda sana mume wangu na ninamheshimu, hili suala linapozungumzwa au kuulizwa linaniumiza sana, haya ni mambo ya muda mrefu na yameshamalizika,” alisema msanii huyo nyota wa kibao cha Malele.
Kwa upande wake Nuh alipotafutwa, simu yake haikupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu jambo hilo pia hakujibu.Hii siyo mara ya kwanza kwa wapenzi hao kukwaruzana, kwani imeshawahi kutokea siku za nyuma hadi kufikia wakati wakatengana.

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget