4:26 PM
NEW NEWS UPDATED
HABARI
5:11 AM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU

OHOOOO! Wakati pazia la mwaka 2014 likifungwa leo, mama la mama, Wema Sepetu ‘Madam’ ameuaga mwaka huo kwa staili ya kilio cha nguvu, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo hatua kwa hatua.
Tukio hilo lililozua maswali mengi bila majibu, lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 29, mwaka huu kwenye shoo ya Madam ya kuuaga mwaka 2014 (Say Good Bye To 2014) iliyofanyika katika Klabu 71, Tegeta-Kibaoni jijini Dar.
SHOO KWANZA
Kabla ya kukutwa na kisanga hicho kwenye shoo hiyo ambayo Madam aliiandaa chini ya Kampuni yake ya Endless Fame, shoo mbalimbali kutoka wasanii kibao wa Bongo Fleva kama Barnaba, Izo Business, Bob Junior na wengine wengi zilihusika kisha baadaye Wema alipanda jukwaani na kumtambulisha msanii wake mpya ajulikanaye kwa jina la Ally Luna.
TUJIUNGE NAYE
“Ally Luna atasimamiwa shughuli zote za kimuziki na mimi chini ya kampuni yangu Endless Fame, na atapata huduma zote za muhimu kama inavyofanyika kwa msanii wangu wa zamani, Mirrow,” alisikika Wema.
KILIO SASA
Mara baada ya shoo hiyo iliyoambatana na bethidei ya mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown kumalizika, Wema alikutwa na mapaparazi nje ya ukumbi huo akiangua kilio cha nguvu ambacho hakikujulikana moja kwa moja ni cha nini.
MAUMIVU YA MAPENZI?
Hata hivyo mnyetishaji mmoja aliwatonya waandishi wetu kuwa huenda Wema analia na maumivu ya mapenzi hususan akifikiria gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa kwenye siku yake ya kuzaliwa na kusababisha aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alitilie shaka.
“Huenda huyu ana maumivu yake ya mapenzi si bure, pengine ni hili gari alilokuja nalo ndilo linamtesa vilevile,” kilisema chanzo hicho.
AUNT AMBEMBELEZA DK 13
Mapaparazi wetu walimshuhudia shosti wa wa damu wa Madam, mwigizaji Aunt Ezekiel akitumia dakika 13 kumbembeleza staa huyo ambaye juzikati alikuwa nchini Ghana kurekodi sinema na mwigizaji kiwango nchini humo, Van Vicker.
ASEMA KABANWA NA MLANGO
Ili kutaka kujua sababu za Madam kuangua kilio kwa muda mrefu, baada ya kunyamaza, mapaparazi wetu walimvaa Wema na kumuuliza kulikoni? Msikie alivyofunguka:
“Nimeumia kwenye mlango wa gari langu baada ya mtu kufunga mlango wa nyuma na kunibana vidole vyangu vya mkono maana nilipata maumivu nahisi kama vimevunjika maana hapa siwezi hata kushika kitu kabisa hata gari kuendesha siwezi najuta kushikilia mlango wa gari yangu.”
WATU WAPINGA
Licha ya majibu hayo, watu waliosikia jibu hilo hawakuamini ambapo walidai haiwezekani kwa mtu mzima kama yeye kuangua kilio kiasi hicho kwa muda mrefu.
“Hataki tu kuanika ukweli, kuna jambo linamtesa hataki tu kuliweka wazi,” alisikika mmbeya mmoja aliyekuwa eneo hilo.
AMTAJA VAN VICKER KUWAACHANISHA NA DIAMOND
Katika hatua nyingine, Wema alipoulizwa sababu za kumwagana na Diamond, alisema pamoja na sababu nyingine, Van Vicker alihusika kuwafanya wamwagane na mpenzi wake huyo waliyedumu kwenye penzi zito lililokuwa gumzo kila kona ya Bongo.
“Kuna vitu vingi vimechangia lakini Van pia amechangia, alianza ku-like picha zangu, nikamwambia Dai (Diamond), akaniambia achana naye, baadaye tulibadilishana namba, tukawa tunawasiliana.
“Ilipofika wakati amenitaka tufanye kazi pamoja, nilipomwambia Diamond ndiyo matatizo yalipoanzia hadi kufikia hatua ya kuachana,” aliweka nukta Wema.
2:33 PM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU

MENGI yameibuka kufuatia waimba Injili Bongo kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo ndoa zao kuvunjika, madai ya kuchepuka, kupata ujauzito nje ya ndoa na matumizi ya madawa ya kulevya, Uwazi limechimba na kuchimbua.
Mpaka sasa, waimba Injili wanawake wameshakumbwa na mikasa mbalimbali lakini mpya kabisa ni madai ya hivi karibuni kwamba, ndoa ya mwimbaji mwingine, Kabula George imesambaratika.
Kabula George mwaka 2012 alitamba na Albamu ya Nitang’ara Tu! Inadaiwa hayuko kwa mumewe baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka nane!
JANET MREMA ANAUMWA
Huyu aliwahi kuripotiwa na Gazeti la Amani miezi miwili iliyopita kwamba, ndoa yake na mumewe, Jonas Mrema imesambaratika madai makubwa ni mume kutomwamini mkewe huyo na kudai alitoroshwa nyumbani na mchungaji mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyejulikana kwa jina moja la Emmanuel.
Habari mpya ni kwamba kwa sasa hali yake ni tete, anaumwa lakini
wengi wanaamini ugonjwa wake unatokana na mawazo ya kuchanika kwa ndoa
yake.Tayari mwanaume huyo ameshafungua kesi Mahakama ya Kinondoni, Dar
akimlalamikia Mchungaji Emmanuel kumtoroshea mkewe. Anataka fidia ya
pesa ambazo mahakama itaamua kama itaona ni sahihi.Huyu aliwahi kuripotiwa na Gazeti la Amani miezi miwili iliyopita kwamba, ndoa yake na mumewe, Jonas Mrema imesambaratika madai makubwa ni mume kutomwamini mkewe huyo na kudai alitoroshwa nyumbani na mchungaji mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyejulikana kwa jina moja la Emmanuel.
BAHATI BUKUKU
Huyu ni mwimba Injili mkongwe Bongo. Ndoa yake na Daniel Basila ilivunjika mwaka 2005, mume alimtuhumu Bahati kutoroshwa nyumbani na mzungu mmoja ambaye hakumtaja jina.
Baadaye Bahati alikanusha, akasema aliamua kuondoka nyumbani kwa Daniel kutokana na manyanyaso mengi. Alishindwa kuvumilia. Mpaka sasa, Bahati hayuko kwenye ndoa.
NEEMA MWAIPOPOHuyu ni mwimba Injili mkongwe Bongo. Ndoa yake na Daniel Basila ilivunjika mwaka 2005, mume alimtuhumu Bahati kutoroshwa nyumbani na mzungu mmoja ambaye hakumtaja jina.
Baadaye Bahati alikanusha, akasema aliamua kuondoka nyumbani kwa Daniel kutokana na manyanyaso mengi. Alishindwa kuvumilia. Mpaka sasa, Bahati hayuko kwenye ndoa.
Alipovuma sana na wimbo wa Sipati Picha alikuwa akijulikana kwa jina la Neema Mushi. Mumewe ndiye Mushi. Baadaye, ndoa yake ilivunjika, akarudia jina la ukoo wake, Mwaipopo. Akatoa albamu inaitwa Raha Jipe Mwenyewe.
ROSE MHANDO
Rose Mhando ndiyo anavyojulikana na wengi. Jina la baba yake ni Athuman. Familia yake yote ni ya Kiislam.
Majanga yake makubwa ni kuzaa watoto watatu pasipokuwa na ndoa. Lakini kwa sasa ana mimba tena, ina maana ni ya mtoto wa nne! Ilishawahi kuandikwa kuwa, kila mtoto ana baba yake!
Lakini pia, Rose aliwahi kudaiwa kubwia ‘unga’ hali inayosemekana kumpotezea utendaji wa huduma.
FLORA MBASHA
Huduma yake kwa sasa ni kama imesimama baada ya ndoa yake na mumewe, Emmanuel Mbasha kuparaganyika!Kwa sasa, Flora yuko mahakamani akimdai talaka mumewe huyo kwa madai kwamba, kwa kipindi chote cha ndoa yao, alikuwa mtu wa kupigwa mara kwa mara!
CHRISTINA SHUSHO!
Na yeye ni mwimba Injili maarufu. Kwa miaka ya hivi karibuni ni kama amezimika! Ilidaiwa naye ndoa yake ina misukosuko ya mara kwa mara. Uwazi liliwahi kumfuata nyumbani kwake, Tabata-Chang’ombe, Dar ili kuujua ukweli wa ndoa yake kukumbwa na upepo wa kisulisuli, msichana wa kazi aliyefungua geti alisema:
“Dada yupo kwenye kikao cha usuluhishi, kuna mchungaji kaja.”
Sarah Mvungi
Ni muimba Injili aliyetokea kwenye fani ya maigizo. ana watoto wawili, kila mmoja ana baba yake. Hana ndoa lakini anatoa huduma ya Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji.
JENNIFER MGENDI
Huyu kidogo Uwazi limepekua maisha yake na kubaini kwamba, yemejaa uadilifu. Ndoa yake haikuwahi kudaiwa kukumbwa na kimbunga cha kusambaratika wala kutengana.
Jennifer Mgendi.
MCHUNGAJI ATOA NENOHuyu kidogo Uwazi limepekua maisha yake na kubaini kwamba, yemejaa uadilifu. Ndoa yake haikuwahi kudaiwa kukumbwa na kimbunga cha kusambaratika wala kutengana.
Mchungaji mmoja wa Kanisa la Evangelical Asemblies of God Tanzania (EAGT) ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema:“Nawaomba hao waimbaji wa kike, hasa wanaodai talaka au walioshindwa kuvumilia maisha ya kwenye ndoa wasome maandiko, mbona yako wazi sana.
“Mimi natabiri kwamba, muziki wa Injili unaporomoka na utazidi kuporomoka kwani shetani amefanikiwa kuwashika waimbaji kwa kusambaratisha ndoa zao kwanza ili washindwe kutoa huduma ya kiroho, maana utahubirije Neno la Mungu wakati wewe linakushinda kulitekeleza?”
KUNA NINI KWENYE INJILI?
Ni swali la kujiuliza sana, ni kwa nini maisha ya waimba Injili, hususan wanawake yako hivi? Mtu anayetoa huduma ya kiroho anapofikia hatua ya kusema
1:01 AM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU
10:53 PM
NEW NEWS UPDATED
HABARI





Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
9:43 PM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU
MWANAMUZIKI Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'
usiku wa kuamkia leo ametwaa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika
Mashariki (Best Male Artist in East Africa) kutoka Tuzo za 2014 AFRIMA
zilizofanyika huko jijini Lagos nchini Nigeria.
Mwanadada Vanessa Mdee yeye ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki (Best Female Artist in East Africa).Tuzo ya Diamond imepokelewa na mwanamuziki Peter Msechu aliyekuwepo katika zoezi hilo la utoaji tuzo maana na yeye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo.
Vanessa Mdee akiwa na tuzo yake ya Best Female Artist in East Africa.
MWANAMUZIKI Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'
usiku wa kuamkia leo ametwaa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika
Mashariki (Best Male Artist in East Africa) kutoka Tuzo za 2014 AFRIMA
zilizofanyika huko jijini Lagos nchini Nigeria.
Mwanadada Vanessa Mdee yeye ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki (Best Female Artist in East Africa).Tuzo ya Diamond imepokelewa na mwanamuziki Peter Msechu aliyekuwepo katika zoezi hilo la utoaji tuzo maana na yeye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo.
10:24 PM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU
Stori: Gladness Mallya
MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Baby Madaha alisema ‘hobi’ yake ni mapenzi japokuwa anapenda muziki lakini haifikii jinsi anavyoyapenda mapenzi kwani yanampumzisha akili yake na kumfurahisha moyo wake pia.
“Ukweli napenda mapenzi kuliko kitu chochote ila sipendi kuzinguliwa na wanaume, ninapenda muziki, filamu lakini haviwezi kufikia mapenzi kwani ndiyo kila kitu kwangu na yananipa starehe kuliko kitu chochote hapa duniani,” alisema Baby Madaha.
MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Baby Madaha alisema ‘hobi’ yake ni mapenzi japokuwa anapenda muziki lakini haifikii jinsi anavyoyapenda mapenzi kwani yanampumzisha akili yake na kumfurahisha moyo wake pia.
“Ukweli napenda mapenzi kuliko kitu chochote ila sipendi kuzinguliwa na wanaume, ninapenda muziki, filamu lakini haviwezi kufikia mapenzi kwani ndiyo kila kitu kwangu na yananipa starehe kuliko kitu chochote hapa duniani,” alisema Baby Madaha.
11:48 AM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU
Stori: Mayasa Mariwata na Hamida Hassan
MKE wa muandaaji mahiri wa filamu George Tyson, Beatrice Shayo amefanikiwa kushinda kesi na kuwa msimamizi wa mirathi baada ya mtafaruku mkubwa uliotokea wa kugombea mali na mwanadada aliyekuwa akiishi na msanii huyo kipindi cha mwisho cha uhai wake, Lucy Sepetu.
Akizungumzia ishu hiyo Beatrice alisema anashukuru Mungu amempigania maana ndugu wengi wa mume hawakuwa upande wake, wengi wao walimuunga mkono Lucy lakini Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imempitisha kuwa msimamizi wa mirathi.
“Nililia sana na kumuomba Mungu kila kukicha kutokana na hili, nashukuru nimeshinda kesi na kuwa msimamizi wa mirathi yakiwemo mashamba, kiwanja, magari mawili na akaunti benki na hivi vyote navisimamia kwa ajili ya watoto wake watatu, ambao ni mwanangu, wa Monalisa na mwingine ambaye aliibuka baada ya kifo cha mume wangu,” alisema Beatrice.
MKE wa muandaaji mahiri wa filamu George Tyson, Beatrice Shayo amefanikiwa kushinda kesi na kuwa msimamizi wa mirathi baada ya mtafaruku mkubwa uliotokea wa kugombea mali na mwanadada aliyekuwa akiishi na msanii huyo kipindi cha mwisho cha uhai wake, Lucy Sepetu.
Akizungumzia ishu hiyo Beatrice alisema anashukuru Mungu amempigania maana ndugu wengi wa mume hawakuwa upande wake, wengi wao walimuunga mkono Lucy lakini Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imempitisha kuwa msimamizi wa mirathi.
“Nililia sana na kumuomba Mungu kila kukicha kutokana na hili, nashukuru nimeshinda kesi na kuwa msimamizi wa mirathi yakiwemo mashamba, kiwanja, magari mawili na akaunti benki na hivi vyote navisimamia kwa ajili ya watoto wake watatu, ambao ni mwanangu, wa Monalisa na mwingine ambaye aliibuka baada ya kifo cha mume wangu,” alisema Beatrice.
3:38 AM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU
Stori: Imelda Mtema
STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma, ametamka hadharani kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Wastara alisema kuna maneno mengi yanasemwa kuwa ana uhusiano na mtu ndani ya kundi hilo kitu ambacho si sahihi, atamuanika mrithi wa marehemu Sajuki siku si nyingi.
“Unajua muda utafika tu lakini kwa hivi sasa sina bwana wala sihitaji mtu yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie na mtu ambaye ataishi na mimi muda ukifika nitawatambulisha na kila mmoja atamjua na siyo mtu kunitabiria au kubuni nitamuweka wazi muda si mrefu,” alisema Wastara.
STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma, ametamka hadharani kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Wastara alisema kuna maneno mengi yanasemwa kuwa ana uhusiano na mtu ndani ya kundi hilo kitu ambacho si sahihi, atamuanika mrithi wa marehemu Sajuki siku si nyingi.
“Unajua muda utafika tu lakini kwa hivi sasa sina bwana wala sihitaji mtu yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie na mtu ambaye ataishi na mimi muda ukifika nitawatambulisha na kila mmoja atamjua na siyo mtu kunitabiria au kubuni nitamuweka wazi muda si mrefu,” alisema Wastara.
11:01 PM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU

BAADA ya kudaiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa alichoropoa mimba zake mbili, mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kujibu mapigo kwamba mwanamuziki huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
Akizungumza na GlobalTV Online kwenye ofisi za gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar, hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.
“Sikukaa sana akaniletea maneno…oooh mara hivi mara vile…eti imetoka. Nikasema poa, labda haikuwa riziki. Nikampa ya pili, nayo pia akatoa. Nikasema bora niachane naye na huo ndiyo ukawa mwisho wa mimi na Penny.”
KILICHOFUATA
Baada ya habari hiyo kuchapishwa kwenye gazeti ndugu la hili, Amani wiki iliyopita, Penny alijibu mapigo na kudai kwamba ni kweli staa huyo alikuwa akimridhisha kimapenzi lakini hakuwa na uwezo wa kumpachika mimba kama alivyodai.“Diamond ni mwanaume kama wanaume wengine lakini hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, muulizeni vizuri tatizo ni nini,” alisema Penny.
DIAMOND ANASEMAJE?Baada ya habari hiyo kuchapishwa kwenye gazeti ndugu la hili, Amani wiki iliyopita, Penny alijibu mapigo na kudai kwamba ni kweli staa huyo alikuwa akimridhisha kimapenzi lakini hakuwa na uwezo wa kumpachika mimba kama alivyodai.“Diamond ni mwanaume kama wanaume wengine lakini hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, muulizeni vizuri tatizo ni nini,” alisema Penny.
Alipofikishiwa taarifa hizo, Diamond hakutaka kufunguka kwa madai kwamba kuna vitu huwa hataki kuvisema kwa kuwa ni mtoto wa kiume na huwa anahifadhi siri nyingi za wanawake.
DIAMOND ANA TATIZO?
Kwa mujibu wa Penny ni kwamba alikuwa akimridhisha vizuri kimapenzi hivyo hana tatizo la nguvu za kiume isipokuwa hawezi kumpa mwanamke kibendi.
KITAALAM ZAIDI
Akizungumzia tatizo la Diamond (kama maelezo ya Penny ni kweli), mtaalam wa masula ya tiba ya uzazi wa gazeti hili (jina tunalo) alisema kuwa mwanaume anaweza kumridhisha vizuri mwanamke wanapokuwa kitandani isipokuwa akashindwa kumpa ujauzito.
“Tatizo la kutopata ujauzito, maana yake mume na mke walio katika
uhusiano wa kutafuta mtoto ndani ya mwaka mmoja, lakini
wameshindwa.“Inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani wa
kiwango cha chini ni mwaka mmoja.“Ni tatizo kubwa katika jamii kwani
kila mmoja anataka afikie malengo ya kuwa na familia kama anavyotaka
Diamond.“Mwanamke na mwanaume wote wanahusika katika tatizo hili japo
mara nyingi huonekana ni la mwanamke.Akizungumzia tatizo la Diamond (kama maelezo ya Penny ni kweli), mtaalam wa masula ya tiba ya uzazi wa gazeti hili (jina tunalo) alisema kuwa mwanaume anaweza kumridhisha vizuri mwanamke wanapokuwa kitandani isipokuwa akashindwa kumpa ujauzito.
8:17 AM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU

Staa anayetamba na ngoma mpya ya ‘Nshumu Nshumu’, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amevamiwa na kung’atwa mguuni na paka anayesadikiwa kuwa na kichaa hivyo kuibua mjadala kuwa endapo hatazingatia chanjo (Vaccination) anahofiwa kufa ndani ya siku 97 tangu alipokutwa na kisanga hicho wiki mbili zilizopita.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Ray C aling’atwa na paka huyo eneo la kutolea dawa za Methadone, ndani ya Hospitali ya Mwananyamala, Dar ambapo alikwenda kunywa dawa ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.
“Ray C alikuwa anakatiza kwa miguu, ghafla akarukiwa na paka na kumng’ang’ania mguu kwa meno.
“Ray C alijaribu kumzuia lakini hakufanikiwa hivyo alisababisha bonge la tafrani. Kama siyo watu kumsaidia yule paka asingetoka mguuni kwake,” alisema shuhuda huyo akisisitiza si bure paka huyo alikuwa na kichaa (rabies).
Ilifahamika kwamba baada ya paka huyo kumvamia, alikimbilia chumba cha matibabu hospitalini hapo ambapo alipata huduma ya kwanza lakini baada ya hapo mguu wake ulianza kuvimba.Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa lilimtafuta Ray C ambaye alikiri kuvamiwa na kung’atwa na paka huyo huku akipinga madai kwamba labda alitumiwa kichawi.
“Kiukweli naendelea vizuri na jeraha limepona baada ya kupatiwa matibabu. Watu wanasema sana lakini mimi sina imani za kichawi,” alisema Ray C.Maelezo ya kitaalam yalionesha kwamba endapo Ray C aling’atwa na paka mwenye kichaa, muda wa kupata virusi vya ugonjwa huo hadi kuanza kwa dalili, kwa kawaida unaweza kuwa kati ya wiki 3 hadi 12.
Maelezo hayo ya kitaalam yalieleza kwamba, mara baada ya kung’atwa, Ray C alipaswa kupata chanjo ya kwanza siku hiyohiyo, chanjo ya pili ilitakiwa iwe baada ya siku tatu, chanjo ya tatu iwe baada ya siku saba na chanjo ya mwisho iwe baada ya siku kumi na nne kama alikuwa hajapata chanjo hiyo kabla.
Kama Ray C aliwahi kuchanjwa dhidi ya ugonjwa huo, alipaswa apewe chanjo mbili, moja palepale (kinga) na nyingine siku ya tatu.Kitaalam ilielezwa kwamba kama Ray C hatafuata utaratibu huo wa chanjo, atakaa kati ya siku 21 hadi 90 ambapo dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa zitakuwa zimeanza kuonekana, ukijumlisha na siku saba za kuumwa basi atakiona kifo ndani ya siku 97 hivyo cha msingi ni kuzingatia chanjo.
Dalili za mtu mwenye ugonjwa huo ambao kiwango cha kuua ni asilimia 100, ni pamoja na homa kali, kuumwa kichwa, kuvimba na kuwashwa koo.
Nyingine ni kuwa mwoga, kuchanganyikiwa, kuwa na tabia zisizo za kawaida, maumivu, kuona vitu ambavyo havipo (maruweruwe), kujifichaficha kwenye kona au kukimbia, kuogopa maji (hydrophobia), mwili kupooza na kushindwa kula. Nyingine ni mgonjwa kushtushwa na mwanga na kelele, kupoteza fahamu na mwisho hupatwa na mauti.
Kwa mujibu wa wataalam hao, muongozo unaojitosheleza wa kupambana na ugonjwa huo ni pamoja na kutoa taarifa ya mnyama (mbwa au paka) anayehisiwa kuwa na kichaa na kumuangamiza haraka iwezekanavyo kabla hajasababisha madhara zaidi.
Pia watu wanashauriwa kuwachanja mbwa au paka wote kwa wakati mmoja na kuendelea kuwachanja watakaozaliwa huku wakidhibiti mbwa wanaotangatanga na kuwaua mbwa wote ambao hawajachanjwa.
11:16 PM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU
4:09 AM
NEW NEWS UPDATED
UDAKU
Subscribe to:
Posts (Atom)