Aliyekuwa
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Warioba akiwasili jioni ya leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest
jijini mwanza.
Umati wa watu waliojitokeza katika mdahalo wa Katiba katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini mwanza.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji msitaafu
Joseph Sinde warioba amewahutubia wananchi jijini Mwanza kuhusiana na
katiba inayopendekezwa na kuwashauri wananchi hao kuisoma kwa umakini
kwanza kabla ya kuipigia kura kwani kuna baadhi ya vipengele
vimentofolewa katika katiba hiyo.
Akizungumza katika mdahalo maalum ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere katika hotel ya Gold Crest Warioba amesema
kuwa watanzania kwa pamoja wapige kura ya ndiyo kama yale
waliyoyapendekeza yamo kwenye katiba na wapige kura ya hapana kutokana
na kuwa yale waliyoya pendekeza hayapo katika katiba hiyo.