
Maiti
ya mtoto mchanga ikiwa imetelekezwa kama ilivyokutwa na wakazi wa eneo
la Airpot jijini Mbeya(Picha kwa hisani ya mmoja wa wakazi wa eneo hilo)
MWANAMKE asiyefahamika ametupa mtoto mchanga katika Dampo
la taka lililopo katika eneo la Airpot jijini Mbeya jirani na kilipo chuo cha
uhasibu(TIA) tawi la Mbeya.
Wakazi wa maeneo ya jirani na dampo hilo wanasema
waliikuta maiti ya kichanga hicho ikiwa imetelekezwa hapo lakini inasadikiwa
kuwa kabla ya kutupwa mtoto huyo alikuwa hai.
Hili si tukio la kwanza kwa maiti za vichanga na pia
vichanga vilivyo hai kukutwa vimetelekezwa kwenye dampo hili.Baadhi ya wakazi
wa maeneo ya jirani na dampo hili wanahusisha matukio ya utupaji watoto
wachanga na pia maiti za watoto hao na wanafunzi wa chuo cha TIA.