STAA wa filamu Will Smith na mkewe Jada Pinkett wanataraji
kusherehekea miaka 20 katika uhusiano wao mbali na kuwa wanandoa hao
walisherehekea miaka 17 ya ndoa yao Desemba 31, mwaka jana.
Jada mwenye umri wa miaka 43, aliandika katika ukurasa wake wa
Facebook kuhusu uhusiano wake na Will huku akielezea matunda ya
mahusiano hayo wakiwemo watoto wao
Willow na Jaden Smith na jinsi walivyoweza kudumu katika upendo na kuvumiliana.
Aliandika hivi: Desemba 31, mwaka jana, nilisherehekea miaka 17 ya
ndoa. Mwezi Februari mwaka huu nitatimiza miaka 20 tangu nilipoamua
kuanza maisha na Will. Nimejifunza kuwa muungano wa watu wawili ni
muujiza wa kweli na watoto ndiyo matunda ya muujiza huo.
Kwa jinsi ninavyoendelea kuupanda mlima huu wa upendo na muungano,
ninahamasika kuona yote ambayo yeye na mimi tumetengeneza tukiwa
kileleni mwa mlima huo. Aliandika Jada katika sehemu ya ujumbe huo.