
Vitu
vya kumbukumbu vya aliyekuwa rais wa 16 wa Marekani Abraham Lincoln
vimeuzwa katika mnada mjini Dallas nchini Marekani na kupata dola
800,000.
Msokoto
mmoja wa nywele za rais huyo aliyeuawa umeuzwa kwa dola 25,000 lakini
barua iliokiri kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe havikuwa vizuri
haikuuzwa.
Barua
iliotiwa sahihi na naibu wake John Wlkes Booth iliuzwa kwa dola 30,000
huku agizo lake la kijeshi likitia kibindoni dola 21,250.

Ukusanyaji wa vitu hivyo 300 ulianzishwa mwaka 1963 na mmiliki wa jumba la sanaa Donald Dow aliyefariki miaka mitano iliopita.
Mwanawe Greg amesema kuwa ni wakati wakusanyaji wengine wapate fursa ya kuifurahia.
Amesema
kuwa babaake alikuwa ameanza ukusanyaji huo kutokana na maslahi yake
katika vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na historia ya kijeshi,lakini
baadaye alikuwa na hamu na Lincoln na mauaji yake.