Stori: Mwandishi Wetu/Risasi
MWANADADA
asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa
sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi
yao.
Chanzo makini kilicho karibu na Wema kilieleza kwamba, mwanadada huyo
kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu huku akijutia mimba aliyopewa na
Kanumba ambayo ilichoropoka kwa bahati mbaya na huyo ndiye mwanaume
pekee aliyewahi kumpa ujauzito.
“Yaani Wema anajutia kweli kwamba kwa nini hakuzaa na Kanumba kwani
ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito ambapo kwa sasa anatafuta
mtoto lakini hapati, yaani yupo kwenye wakati mgumu sana akikuelezea
mwenyewe unaweza kulia kwani ana simulizi ya kusikitisha kuhusu maisha
yake na Kanumba.
“Hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani
kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa
Kanumba anateseka kweli moyoni,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Wema kuhusu ishu hiyo alikiri na kuonesha namna gani anateseka moyoni.
“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena.
Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na
mimi itatokea nitapata,” alisema Wema.