Msanii huyo wa kike aliyevuma kwa wimbo wa ‘Johnny’, alitoa kauli yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambako aliandika: “Mungu ambariki. Mbingu imepata malaika mwenye thamani kubwa,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha ya baba yake.

“Asanteni sana kwa ujumbe wenu. Mipango ya mazishi itatolewa wakati ukifika,” aliandika staa huyo.